Toa zakaah itapofika mwaka na usisubiri Ramadhaan?

Swali: Kuna ubora kwa kutoa zakaah katika Ramadhaan juu ya miezi mingine pamoja na kwamba ni wajibu ikitimiza masharti?

Jibu: Lililo la wajibu juu ya zakaah mtu aitoe pale itapotimiza mwaka. Mtu asisubiri Ramadhaan. Akipenda kuitoa katika Ramadhaan ilihali imekwishatangulia kufikisha mwaka, basi amuombe Allaah msamaha juu ya kuichelewesha. Hakuna neno akatanguliza zakaah inayokuja katika Ramadhaan. Hapa ni kwa njia ya zama. Hapana shaka kwamba kutoa katika Ramadhaan ndio bora zaidi. Lakini wakati fulani zakaah na swadaqah mbali na Ramadhaan inakuwa ndio bora zaidi. Kwa sababu mafukara wanakuwa ni wahitaji zaidi mbali na Ramadhaan, kama inavyotambulika. Kwa sababu katika Ramadhaan zakaah na swadaqah zinakuwa nyingi ambapo mafukara wanakuwa na kitu katika utajiri. Lakini mbali na Ramadhaan huenda wakawa ni wahitaji zaidi.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa´ ash-Shahriy (70) http://binothaimeen.net/content/1574
  • Imechapishwa: 10/03/2020