Swali: Mtu ambaye yuko na dishi/king´amuzi ni vipi atajinasua nacho ili aitakase dhimma yake?

Jibu: Ni wajibu kwetu kutahadharisha dhidi ya ving´amuzi hivi. Tunaona kuwa yule ambaye yuko na kitu katika hayo basi haitakasiki dhimma yake isipokuwa kwa kuivunja kabisa. Kwa sababu akikibakiza ni tatizo. Akikiuza amemsalitisha yule mnunuaji juu ya kukitumia[1]. Hakuna njia salama isipokuwa kwa kukivunja. Tunataraji Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) atampa badala bora yule mwenye kukivunja. Kwa sababu amekiacha kitu kwa ajili ya Allaah (´Azza wa Jall).

[1] Tazama https://firqatunnajia.com/inafaa-kumuuzia-kafiri-kitu-cha-haramu-kama-tv-au-dishi/

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa’ ash-Shahriy (42) http://binothaimeen.net/content/982
  • Imechapishwa: 28/12/2018