Swali: Ni yapi maoni yako kwa wale ambao Ujerumani na sehemu nyinginezo wanawaita Salafiyyuun “Madaakhilah” na wanawatuhumu kwamba wamefarikisha Ummah, wanadai Salafiyyah na kwamba hawajui jengine zaidi ya kutukana tu na kujeruhi?

Jibu: Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah hawamfuati yeyote mwingine zaidi ya Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Wanafuata Qur-aan na Sunnah katika ´Aqiydah, mfumo, siasa, tabia na mambo mengine katika maisha. Wanafuata dalili na hawazushi. Kuanzia pwenti hii, utahadharisho wa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) juu ya Ahl-ul-Bid´ah na utahadharisho wa Salaf kwao, wao ni wenye kushikamana barabara na mfumo huu. Yule anayeenda kinyume nao na kuwaita kuwa ni “Jaamiyyah” au “Madaakhilah” ni mpotevu. Kwa kuwa anaipiga vita Sunnah na mfumo wa Salaf.

Ni wajibu wao kumcha Allaah juu ya nafsi zao na waache kupeana majina mabaya ya bandia. Badala yake wawe wakweli na waseme kauli ya sawasawa:

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اتَّقُوا اللَّـهَ وَقُولُوا قَوْلًا سَدِيدًا يُصْلِحْ لَكُمْ أَعْمَالَكُمْ وَيَغْفِرْ لَكُمْ ذُنُوبَكُمْ ۗ وَمَن يُطِعِ اللَّـهَ وَرَسُولَهُ فَقَدْ فَازَ فَوْزًا عَظِيمًا

“Enyi mlaomini! Mcheni Allaah na semeni kauli ya sawasawa. Atakutengenezeeni matendo yenu na atakusameheni madhambi yenu; na anayemtii Allaah na Mtume Wake, basi kwa hakika amefanikiwa mafaniko makubwa.” (33:70-71)

Je, wao wako dhidi ya Salafiyyuun na kuwaita kwa majina haya ya bandia kwa ajili tu wameshikamana barabara na Qur-aan na Sunnah? Ni Bid´ah zipi walizonazo mpaka muiwaite kuwa ni “Jaamiyyah” na “Madaakhilah”? Wana Bid´ah zipi?

Tunajua jinsi Jamaa´at-ut-Tabliygh, al-Ikhwaan al-Muslimuun na Qutbiyyuun wamevyozusha na kupotea katika mambo ya msingi na matawi. Tunawanasihi na kuwabainishia haki. Yule ambaye anawafikishwa na Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala), anarudi katika haki na kufuata njia ya Salaf. Na yule ambaye Allaah (Tabaarak wa Ta´ala) amemuacha na hamtakii kheri, anamuacha na kuzidi kutumbukia katika upotevu na dhuluma zaidi.

  • Mfasiri: Firqatunnajia.com