Tetesi Za Kuwepo Kaburi Ndani Ya Msikiti

Swali: Ikiwa kuna msikiti ambao kunasemwa una kaburi. Lakini hata hivyo haijathibitishwa. Inajuzu kuswali kwenye msikiti huu?

Jibu: Asli ni mtu kwenda huko na kuswali. Maadamu hakujathibitishwa kuwa kuna kaburi mtu aende na kuswali. Lau kungelikuwa kaburi ingejulikana.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Fath-il-Majiyd (34) http://alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/fathulmajid-17-11-1436-01.mp3
  • Imechapishwa: 12/02/2017