Swali: Mume wangu anapuuzia swalah. Wakati fulani anaswali na wakati mwingine anaacha kuswali. Tumeshazaa naye watoto watatu. Ni kipi kinachonilazimu juu ya mume huyu?

Jibu: Ni wajibu kumnasihi. Akitubu kwa Allaah na akachunga swalah ni vizuri. Vinginevyo muombe kutengana naye. Haijuzu kubaki naye ilihali haswali. Kwa sababu ni kafiri. Mpaka pale atakapotubia kwa Allaah. Akitubu na akachunga swalah baki naye. Ama akiendelea kuacha swalah kwa makusudi ni kafiri na wala haijuzu kwako kubaki pamoja naye. Muombe kutengana naye.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Thalaathat-il-Usuwl (07) http://ajurry.com/safrawy/chorohat-elakida/charh-el-osol-el-thalatha/charh-fwzan/07.mp3
  • Imechapishwa: 25/01/2019