Tazama kile unachotaka kununua


Swali: Mimi hununua bidhaa zikiwa zimefungwa kwenye pakiti vizuri. Najua kuwa kwenye pakiti hizi kuna mavazi yaliyotumiwa lakini sifungui kabla ya kununua. Je, kitendo changu hichi ni sahihi? Je, ununuzi huu unafaa?

Jibu: Si sahihi kununua kitu kisichojulikana. Ni lazima ufungue pakiti, utazame mavazi yaliyomo ndani na uyapekue. Ni lazima ujue. Usinunue kitu ambacho hujui kuna nini ndani yake. Bei  ni lazima iwe yenye kutambulika na bidhaa iwe yenye kutambulika. Hii ni sharti moja wapo ya kusihi kwa biashara.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Ighaathat-il-Lahfaan (85) http://alfawzan.af.org.sa/ar/node/17635
  • Imechapishwa: 23/06/2018