Miongoni mwa athari mbaya za wasomi wa falsafa na wale walioathirika na falsafa zao (kama mfano wa huyu as-Saqqaaf ambaye ameghurika nao) ni kwamba hawazingatii kabisa bidii iliofanywa na maimamu, wanachuoni na wenye kujeruhi katika Hadiyth. Wanayasaliti matamanio yao juu ya Hadiyth ambazo wanachuoni wamezisahihisha au wamezidhoofisha. Wanazikubali na kuzitumia zile zinazoendana na wao, japokuwa zitakuwa ni dhaifu, na wanazitupilia mbali zile ambazo haziendani nao, japokuwa zitakuwa ni Swahiyh. Haya ni mambo yanayoonekana kwa uwazi kabisa kwa wale watangu wao na wale waliokuja nyuma. Mfano wa wazi juu ya hilo ni Shaykh al-Kawthariy na ´Abdullaah al-Ghumaariy. Wanaona kuwa Hadiyth ya yule mjakazi:

“Allaah yuko wapi?” Akasema: “Juu ya mbingu.” Ndipo akasema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam): “Mwache huru. Kwani hakika ni muumini.”

ni dhaifu. Wakafuatwa kichwa mchunga na yule mwangamivu as-Saqqaaf. Bali yeye aliwazidi ukandamizaji na ghururi na akasema:

“Sisi tunasema kwa kukata kabisa ya kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) hakusema “Allaah yuko wapi?”[1]

na:

“Tamko hilo ni la kutisha.”[2]

Hivi ndivo anavosema mpumbavu. Yeye anajua kuwa wanachuoni wameafikiana juu ya usahihi wa Hadiyth. Wameikubali katika zama zote. Maimamu wakubwa wameitumia kama hoja. Baadhi yao ni Maalik, ash-Shaafi´iy na Ahmad. Muslim, Abu ´Awaanah, Ibn-ul-Jaaruud, Ibn Khuzaymah, Ibn Hibbaan kisha wakakubaliana kuisahihisha akiwemo al-Bayhaqiy, al-Baghawiy, Ibn-ul-Jawziy, adh-Dhahabiy na al-´Asqalaaniy. Baadhi ya hawa wao wenyewe wanazipindisha sifa za Allaah.

Kitu gani atachosema muisamu mwenye busara juu ya mjinga, mkanushaji na mtu mkaidi ambaye anaenda kinyume na maimamu hawa na anasema kuwa tamko la Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ambalo wamelisahihisha kwamba linatisha? Bali anawaita wale ambao wanaitaja Hadiyth hii ya kinabii kwamba ni Mujassimah[3].

[1] Taaliki ya ”Daf´ Shubah-it-Tashbiyh”, uk. 108

[2] Taaliki ya ”Daf´ Shubah-it-Tashbiyh”, uk. 188

[3] Tazama ukurasa wa 187.

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Silsilat-ul-Ahaadiyth as-Swahiyhah (1/1/486)
  • Imechapishwa: 21/05/2019