Swali: Nilikuwa na janaba na kabla ya kuingia msikitini nikafanya Tayammum na kuswali. Je, swalah yangu inakubaliwa?

Jibu: Ukiwa ndani ya mji hauna rukhusa ya kufanya hivo. Ukiwa ndani ya mji basi ni lazima kwako kutafuta maji, oege kisha uswali tena. Haijalishi kitu hata kama utapitwa na swalah ya mkusanyiko. Huna rukhusa ya kufanya Tayammum isipokuwa utaposhindwa kuyatumia maji au ukakosa maji mjini. Huku ni kuchukulia wepesi. Vipi utafanya Tayammum ilihali uko ndani ya mji kisha unaswali na huku uko na janaba?

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (07) http://dl.islamweb.net/audiopath/audio/lecturs/aalrrajhee/434/434.mp3
  • Imechapishwa: 14/12/2018