Swali: Baadhi ya watu wanasema kuwa al-Haakimiyyah ndio Uluuhiyyah maalum

Jibu: Hapana. Ambayo ni maalum ni kuacha shirki. al-Haakimiyyah ni katika matawi ya hukumu. Ni wajibu kwa mtawala ahukumu kwayo. Ni wajibu kwa mtawala kuhukumu kwa Shari´ah. Akihukumu kinyume na Shari´ah kwa kukusudia na kwa kuhalalisha anakufuru. Endapo atahukumu kwa matamanio na rushwa inakuwa ni maasi, maovu na kufuru ndogo.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Kashf-ish-Shubuhaat, uk. 75
  • Imechapishwa: 30/11/2016