Swali: Suufiyyah wanatumia hoja kwa Hadiyth kuhusu Malaika wawili wanapomuhoji mtu ndani ya kaburi kwa kumuuliza “Ni nani Mola Wako?” ya kwamba Tawhiyd inayotakikana ni Tawhiyr-ur-Rubuubiyyah. Vipi mtu atajibu hili?

Jibu: Ametakasika Allaah. Ni kwa nini ameacha “Ni ipi dini yako?” Hii ndio Tawhiyd. Ni nani Mola Wako na ni ipi dini yako. Hii ndio maana ya nashuhudia ya kwamba hakuna muabudiwa wa haki isipokuwa Allaah na kwamba Muhammad ni Mtume wa Allaah. Anachukua sehemu ya maneno na kuacha mengine?

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Qaa´idah Jaliylah fiyt-Tawassul wal-Wasiylah (07) http://alfawzan.af.org.sa/node/2122
  • Imechapishwa: 02/07/2020