Tawbah ya ambaye alikuwa anafanya kazi katika benki ya ribaa

Swali: Nilifanya kazi katika benki ya ribaa na nikachuma mali. Vipi nitatubu tawbah ya kweli pamoja na kuzingatia kwamba hivi sasa nafanya kazi ya halali na nimeacha kazi ile ya haramu?

Jibu: Nataraji kwamba tawbah yake itafuta yale yaliyotangulia. Kwa sababu Allaah (Ta´ala) amesema:

فَمَن جَاءَهُ مَوْعِظَةٌ مِّن رَّبِّهِ فَانتَهَىٰ فَلَهُ مَا سَلَفَ وَأَمْرُهُ إِلَى اللَّـهِ

“Yule atakayefikiwa na mawaidha kutoka kwa Mola wake ambapo akakoma, basi ni yake yale yaliyopita na jambo lake iko kwa Allaah.”[1]

Allaah amemruhusu yale yaliyopita. Vilevile amesema:

وَأَمْرُهُ إِلَى اللَّـهِ

“… na jambo lake liko kwa Allaah.”

Isipokuwa ikiwa kama ile ribaa haikuchukuliwa. Mtu asiichukue baada ya kutubu. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Ribaa ya kipindi cha kikafiri imekwisha. Ribaa ya kwanza ninayoiangusha ni ribaa yetu ambayo ni ya ´Abbaas bin ´Abdil-Muttwalib. Zote naziangusha.”[2]

Lakini akiichukua basi asibaki nayo. Bali aitoe swadaqah kwa ajili ya kujikwamua nayo.

[1] 02:275

[2] Muslim (1218).

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa’ ash-Shahriy (47) http://binothaimeen.net/content/1074
  • Imechapishwa: 04/07/2020