Tawbah Inapaswa Kuwa Kwa Ajili Ya Allaah

Swali: Je, Tawbah ya mtu inakubaliwa ikiwa sababu yake ni kwa ajili ya kheri atayoipata katika dunia? Kwa mfano mtu anatubu kuvuta sigara ili Allaah Aweze kumpa mafanikio na masomo yake au akatubu kusikiliza muziki ili Allaah Aweze kumponya maradhi yake na mfano wa hayo.

Jibu: Tawbah inapaswa kuwa kwa ajili ya Allaah (´Azza wa Jall). Haitakiwi kuwa katika mambo ya kidunia. Mtu anatakiwa kutubu kwa ajili ya Allaah. Tawbah ni ´ibaadah kama jinsi zilivo ´ibaadah nyinginezo. Kama jinsi haijuzu kwake kuswali ili aweze kupata mali na kufuzu mtihani, kadhalika Tawbah haijuzu. ´Ibaadah inatakiwa iwe kwa ajili ya Allaah.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajhiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://subulsalam.com/play.php?catsmktba=13967
  • Imechapishwa: 01/05/2015