Tawbah ina sifa maalum katika Ramadhaan?

Swali: Je, tawbah ina sifa maalum katika Ramadhaan au inafanywa nyakati zote?

Jibu: Tawbah inakuwa katika kila wakati. Tawbah katika Ramadhaan ina sifa maalum ikiwa mtu amenuia kuendelee juu yake. Asikusudie kutubu katika Ramadhaan peke yake na baadaye akarudi katika matendo yake maovu baada ya Ramadhaan. Mtu kama huyu haikubaliwi tawbah yake. Atubu kwa Allaah katika Ramadhaan na anuie kuendelea juu yake mpaka wakati wa kifo.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://www.youtube.com/watch?v=bh2DpsHpwcU
  • Imechapishwa: 11/05/2020