Tawassul za Bid´ah zinapelekea katika shirki


Swali: Kuomba Du´aa kwa haki ya fulani au kwa jaha ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) au kwa dhati ya viumbe ni njia inayopelekea katika shirki au ni shirki kabisa?

Jibu: Ni Bid´ah. Kuomba Du´aa kwa jaha au kwa haki ya fulani ni Bid´a. Ni njia inayopelekea katika shirki. Ni jambo limekusanya mambo mawili:

1- Ni Bid´ah. Kwa kuwa ni kufanya jambo lisilokuwa na dalili kutoka katika Qur-aan na Sunnah.

2- Ni njia pia inayopelekea katika shirki. Waabudu makaburi hawakutumbukia katika kuyaabudu makaburi isipokuwa ilikuwa ni kwa sababu ya hili. Walianza kwa kutawassul kwao kwanza kisha ndio wakajikurubisha kwao kwa kuwafanyia ´ibaadah na utiifu. Hivyo wakawa wametumbukia kwenye shirki kubwa.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Aqiydat-is-Saffaariniyyah (13) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/sfranih_13.mp3
  • Imechapishwa: 18/06/2018