Tawarruk inakuwa katika swalah zipi?

Swali: Je, Tawarruk inakuwa katika zile swalah za Rak´ah nne pekee? Ni ipi hukumu ya Tawarruk katika swalah za Rak´ah tatu au vilevile katika swalah ya Fajr na swalah ya ijumaa?

Jibu: Tawarruk ni kule kukalia kalio katika Tashahhud ya mwisho na akaielekeza miguu yake miwili upande wa kulia [kwa nyuma]. Jambo hili linakuwa katika swalah ambayo ina Tashahhud mbili kama vile Dhuhr, ´Aswr, ´Ishaa na swalah zenye Rak´ah tatu kama vile Maghrib. Kuhusu swalah za Rak´ah mbili hakuna Tawarruk kwa mujibu wa maoni sahihi. Masuala haya wanachuoni wametofautiana kwayo. Lakini hiki ndicho chenye kutegemewa. Wapo wanachuoni wenye kuona kwamba Tawarruk inakuwa katika zile swalah zilizo na Tashahhud mbili. Maoni ya sawa ni kwamba Tawarruk inakuwa katika Tashahhud ya mwisho katika swalah yenye Rak´ah mbili. Ama kuhusu swalah ya ijumaa, swalah za sunnah na swalah ya Fajr hakuna Tawarruk.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (06) http://dl.islamweb.net/audiopath/audio/lecturs/aalrrajhee/433/433.mp3
  • Imechapishwa: 21/11/2018