Tatizo linalowasumbua kina dada wengi wa Kiislamu

Swali: Ni ipi hukumu kwa mtu ambaye amemuoza msichana wake kwa kafiri pasi na kujua kuwa ni haramu?

Jibu: Ndoa ni batili hata kama alikuwa hajui. Ni lazima kwake kumchukua msichana wake kutoka kwa huyo kafiri:

فَإِنْ عَلِمْتُمُوهُنَّ مُؤْمِنَاتٍ فَلَا تَرْجِعُوهُنَّ إِلَى الْكُفَّارِ ۖ لَا هُنَّ حِلٌّ لَّهُمْ وَلَا هُمْ يَحِلُّونَ لَهُنَّ

”Mkiwatambua kuwa ni waumini wa kike, basi msiwarejeshe [huko Makkah] kwa makafiri; wao [wanawake] si halali kwao [makafiri] na wala wao [waume] si halali kwao [hao wanawake].” (al-Mumtahinah 60:10)

Msiba ni kwamba kuna waislamu wanaoritadi wanabaki pamoja na wanawake zao waislamu. Hili ni jambo linatokea sana. Utamkuta mwanaume anaacha swalah kwa kukusudia, anaitukana dini, anaifanyia shere dini, anafanya moja katika vitenguzi vya Uislamu na mwanamke huyu wa Kiislamu anaendelea kuishi naye kwa kujengea juu ya msingi kwamba mwanzoni alikuwa ni muislamu. Hazindukani juu ya hili. Hili ni tatizo linalowasumbua dada wengi wa Kiislamu wanabaki pamoja na mritadi. Mritadi huyu anakuwa na usimamizi juu yake, anamwita yeye na watoto wake katika kuritadi.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Nawaaqidhl-il-Islaam (08) http://ajurry.com/safrawy/chorohat-elakida/chorohat-nawakid-elislam/charh-salah-fawzan/08.mp3
  • Imechapishwa: 15/02/2019