Tasmiyah chooni kabla ya kutawadha

Swali: Ni ipi hukumu ya mwenye kutawadha ndani ya bafu?

Jibu: Hakuna neno mtu akatawadha bafuni haja ikipelekea kufanya hivo. Mwanzoni mwa wudhuu´ aseme: “ Bismillaah”. Kwa sababu kwa mujibu wa baadhi ya wanazuoni wanaona kuwa kutaja jina la Allaah ni lazima na wengi wao wanaona kuwa ni kitu kimetiliwa mkazo. Kwa hivyo ailete na yataondoka machukizo. Kwa sababu machukizo yanaondoka wakati kunapokuwepo haja ya kutaja jina la Allaah. Mtu ameamrishwa kutaja jina la Allaah mwanzoni mwa wudhuu´. Kwa hivyo ataje jina la Allaah na akamilishe wudhuu´ wake.

Kuhusu kuleta Tashahhud inakuwa baada ya kutoka ile sehemu ya kukidhi haja. Akimaliza kutawadha atoke nje ya alete Tashahhud nje yake.

Ikiwa bafu ni kwa ajili ya kutawadha peke yake (na si kwa ajili ya haja kubwa wala ndogo), maeneo haya hakuna neno akaileta [Tashahhud]. Kwa sababu sio mahali pa kukidhi haja.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (10/28)
  • Imechapishwa: 30/07/2021