Swali: Je, imepokelewa katika swalah mtindo wa kutoa salamu? Ni upi?

Jibu: Iliyokuja ni:

السلام عليكم ورحمة الله

“Amani na rehema za Allaah ziwe juu yenu.”

kuliani na kushotoni. Katika baadhi ya mapokezi imekuja:

السلام عليكم ورحمة الله تعالى وبركاته

“Amani, rehema na baraka za Allaah ziwe juu yenu.”

lakini hata hivyo kuna maneno juu yake ya wanachuoni.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (03) http://audio2.islamweb.net/lecturs/aalrrajhee/430/430.mp3
  • Imechapishwa: 08/04/2018