Tasa kujifunua mbele ya daktari wa kiume kwa sababu ya matibabu

Swali: Ni ipi hukumu ya kumfunulia daktari viungo visivyotakiwa kuonekana kwa sababu ya haja kubwa ya kutibiwa kwa mwanamke ambaye ni tasa na mume analijua hilo?

Jibu: Hakuna neno mwanamke akamfunulia daktari viungo visivyotakiwa kuonekana kwa sababu ya haja. Lakini tunasema kwamba yale ambayo haja imepelekea vifunuliwe kwa njia ya kwamba mwanamke huyo awe ni mwenye kuhitajia ufunuaji huu na wala hakuna madaktari wanawake wenye kufanya kazi hii. Ikiwa hakuna madaktari wa kike wenye kufanya kazi hii basi hakuna neno akajifunua mbele ya daktari wa kiume kutokana na ile haja iliopelekea kufanya hivo[1].

Tazama https://firqatunnajia.com/mwanamke-na-daktari-wa-kiume/

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Nuur ´alaad-Darb (12) http://binothaimeen.net/content/6769
  • Imechapishwa: 24/01/2021