Swali: Mimi nafanya kazi kwenye kiwanda cha biashara kilicho na kituo cha petroli kilicho na duka na kibanda. Pambezoni mwetu uko msikiti mdogo lakini hawaswali Tarawiyh. Baada ya swalah ya ´Ishaa kila mmoja anaenda kazini kwake. Nifanye nini? Punde tu baada ya swalah ya ´Ishaa niswali Tarawiyh peke yangu?

Jibu: Una khiyari kati ya kuswali peke yako na unapata ujira au ukaswali nyumbani kwako. Yote mawili ni mazuri muda wa kuwa hakuna mkusanyiko. Pia ukienda msikitini ni sawa. Kwa sababu Tarawiyh imependekezwa na sio faradhi. Ni sawa ukiswali msikitini au nyumbani kwako au kwenye msikiti mwingine. Yote ni sawa.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Nuur ´alaad-Darb https://binbaz.org.sa/fatwas/18846/%D8%AD%D9%83%D9%85-%D8%B5%D9%84%D8%A7%D8%A9-%D8%A7%D9%84%D8%AA%D8%B1%D8%A7%D9%88%D9%8A%D8%AD-%D9%85%D9%86%D9%81%D8%B1%D8%AF%D8%A7
  • Imechapishwa: 05/05/2020