Tarawiyh mkusanyiko wanawake nyumbani

Swali: Inafaa kwa mwanamke kuswali Tarawiyh katika nyumba isiyokuwa na wanamme akiwa pamoja na kikosi cha dada zake wengine?

Jibu: Ndio, imesuniwa kwao kuswali Tarawiyh au katika zile siku kumi za mwisho. Wanaweza wakaswali mkusanyiko au mmojammoja. Yote mawili ni sawa. Pia wakiswali pamoja na wanamme hali ya kuwa wamejisitiri na wamejihifadhi ni sawa na yote ni mazuri.

Mwendesha kipindi: Akisoma kwa sauti ya juu kiasi cha kwamba haimsikilizishi yeyote?

Jibu: Hakuna neno akasoma kwa sauti ya juu awasikilizishe wanawake wenzake. Anatakiwa kusimama katikati ya safu yao na asisimame mbele yao. Asome kwa sauti yenye kusikika ili wapate kufaidika.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Nuur ´alaad-Darb https://binbaz.org.sa/fatwas/17047/%D8%AD%D9%83%D9%85-%D8%B5%D9%84%D8%A7%D8%A9-%D8%A7%D9%84%D8%AA%D8%B1%D8%A7%D9%88%D9%8A%D8%AD-%D8%AC%D9%85%D8%A7%D8%B9%D8%A9-%D9%84%D9%84%D9%86%D8%B3%D8%A7%D8%A1
  • Imechapishwa: 06/05/2020