Tarawiyh mkusanyiko wanawake nyumbani II

Swali: Nataka kujua namna mwanamke anavoswali swalah ya Tarawiyh kama anaswali peke yake? Je, wanawake wanaweza kuswali mkusanyiko katika nyumba zao?

Jibu: Ndio. Tarawiyh anatakiwa kutoa salamu kila baada ya salamu mbili. Mwanamke mwenziwe anaweza kuwaswalisha na atasimama katikati ya safu yao na asisimame mbele yao. Alete Takbiyr na anyanyue sauti yake juu wakati wa kusoma ili walioko nyuma wapate kufaidika kutoka kwake. Haya yamesuniwa na yamepokelewa kutoka kwa ´Aaishah na wengineo katika wakeze Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kwamba walifanya hivo. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alimwamrisha Umm Waraqah awaongoze watu wa nyumbani kwake kwenye nyumba yake. Kwa hiyo wanawake wakiswali nyumbani swalah ya mkusanyiko katika Ramadhaan au wakati mwingine wanaposwali swalah ya faradhi, basi yote yanafaa na ni sawa.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Nuur ´alaad-Darb https://binbaz.org.sa/fatwas/25474/%D9%83%D9%8A%D9%81%D9%8A%D8%A9-%D8%B5%D9%84%D8%A7%D8%A9-%D8%A7%D9%84%D8%AA%D8%B1%D8%A7%D9%88%D9%8A%D8%AD-%D8%A8%D8%A7%D9%84%D9%86%D8%B3%D8%A8%D8%A9-%D9%84%D9%84%D9%85%D8%B1%D8%A7%D8%A9
  • Imechapishwa: 06/05/2020