Swali: Baadhi ya watu wanapokuwa na baadhi ya maasi kisha wakanasihiwa, wanaashiria mkono wao juu ya kifua kwenye moyo na kusema: “Kitu muhimu ni hiki.”

Ni vipi wataraddiwa aina ya watu kama hawa?

Jibu: Haya yanayofanywa na baadhi ya watu pindi wanaponasihiwa wanasema:

“Taqwa iko hapa.”

ni maneno ya kweli. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Taqwa iko hapa” akaashiria kwenye kifua chake na alisema hivo mara tatu.”

Lakini yule aliyesema:

“Taqwa iko hapa.”

ndiye huyo huyo aliyesema:

“Tanabahini! Hakika kwenye kiwiliwili kuna kiungo; kinaponyooka basi mwili mzima hunyooka, na kinapoharibika mwili mzima huharibika.”

Kujengea juu ya haya kuharibika kwa uinje kunafahamisha kuwa hata ndani pia kumeharibika. Tunamwambia huyu ambaye amesema:

“Taqwa iko hapa.”

lau hichi kilichoko hapa ndani yake kungelikuwa taqwa kweli, basi matendo ya dhahiri tunayoyaona nayo pia yangelikuwa na taqwa. Kwa kuwa moyo ukiwa na uchaji Allaah, basi ni lazima viungo navyo viwe na uchaji Allaah. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“… kinaponyooka basi mwili mzima hunyooka, na kinapoharibika mwili mzima huharibika.”

Hivyo tunakuwa tumebatilisha hoja yake na kumwambia: lau ungelikuwa mkweli ya kwamba moyo wako una taqwa, basi viungo vyako pia vingelikuwa na taqwa.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa’ ash-Shahriy (05)
  • Imechapishwa: 02/05/2020