Taqiyyah kwa mtazamo wa Raafidhwah


Imepokelewa kutoka kwa as-Swaadiq (Radhiya Allaahu ´anh) ambaye amesema:

Taqiyyah [unafiki] ni dini yangu na ni dini ya mababa zangu.”[1]

Kitabu hichi kwa mujibu wao ni kama al-Bukhaariy kwa mujibu wetu. Allaah amemtakasa kutokamana na hayo. Kuna baadhi yao wamefasiri maneno Yake (Ta´ala):

إِنَّ أَكْرَمَكُمْ عِندَ اللَّـهِ أَتْقَاكُمْ

“Aliye mtukufu zaidi miongoni mwenu mbele ya Allaah ni yule mwenye taqwa zaidi kati yenu.” (49:13)

“Ni yule mwenye Taqiyyah sana na kuwaogopa sana watu.”

Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Mwenye kuifasiri Qur-aan kwa maono yake amekufuru.”

[1] Tazama ”al-Kaafiy” ya al-Killiyniy (02/228).

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: ar-Radd ´alaa ar-Raafidhwah, uk. 64
  • Imechapishwa: 14/04/2017