Swali: Sisi katika nchi yetu mtu anapofariki basi anapewa pole kwa kusomwa “al-Faatihah”. Baadhi ya wanazuoni katika nchi yetu wamesema kuwa kutoa pole si jambo linalotegemea dalili kutoka katika Qur-aan na Sunnah wakimaanisha kwamba kitendo hicho kinafaa. Je, maneno yao ni sahihi?

Jibu: Hapana. Hii ni Bid´ah. Tanzia kwa usomaji wa al-Faatihah ni Bid´ah. Haijuzu isipokuwa kwa dalili kutoka katika Qur-aan na Sunnah, kitu ambacho hakina dalili. Tanzia inakuwa kwa kuomba du´aa isemayo:

جبر الله مصيبتك أحسن الله عزاءك وغفر لميتك

“Allaah aunge msiba wako, akufanye kuzuri kutaaziwa kwako na amsamehe maiti wako.”

Hii ndio iliyopokelewa.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (16)
  • Imechapishwa: 02/05/2021