Swali: Je, kule Jibriyl (´alayhis-Salaam) kujifananiza na sura ya mwanaume ni dalili ya yale yanayoitwa hii leo “tamthilia za kiislamu”? Ni ipi hukumu ya tamthilia kwa vile mtu anamwigiza mwengine?

Jibu: Jibriyl (´alayhis-Salaam) alijifananiza na sura ya mwengine kwa sababu Allaah alimpa uwezo wa kufanya hivo.

Kuhusu tamthilia usawa ni kwamba hazijuzu. Dogo liwezalo kusemwa ni kwamba ni uongo. Kwa mfano mtu anajimithilisha kwamba yeye ni ´Umar bin al-Khattwaab au kwamba ni hivi na vile. Haya gogo liwezalo kusemwa ni kwamba ni uongo. Mtu anaweza kuwalingania watu kwa maneno mazuri, anawasifu Maswahabah, anazitaja sifa zao na matendo yao mazuri pasi na tamthilia. Tamthilia ni kufungua mlango wa uongo.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (02) http://audio2.islamweb.net/lecturs/aalrrajhee/429/429.mp3
  • Imechapishwa: 05/02/2018