Talaka za kuandikiana magharibini zinahesabika?

Swali: Mume akipitisha talaka katika moja ya serikali za magharibi kwa njia ya makaratasi peke yake pasi na talaka ya Kishari´ah ambayo kwa mujibu wao huita ´talaka ya kiinchi`. Je, talaka hii inapita?

Jibu: Ndio. Akitamka talaka inapita. Akitamka talaka au akaiandika inapita. Isipokuwa ikiwa kama amelazimishwa juu ya talaka hiyo hapo haipiti. Kadhalika haipiti talaka katika hali ya kutokwa na akili.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Ighaathat-il-Lahfaan (87) https://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/Fathul%20Majd-3-7-1439.mp3
  • Imechapishwa: 11/11/2018