Talaka rejea ndani ya eda ni wajibu kuomba idhini kabla ya kutoka nje

Swali: Ikiwa ni Talaka rejea, je ni lazima kwa mke kumuomba idhini mume wake wakati anapotaka kutoka katika haja zake au na familia yake? Na kama hakufanya hivyo, ni ipi hukumu?

Jibu: Ndio. Maadamu yuko ndani ya eda na ni Talaka rejea, bado ni mume wake. Asitoke isipokuwa kwa idhini yake, kwa kuwa bado ni mume wake. Hivyo, asitoke isipokuwa mpaka kwa idhini yake.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: www.alfawzan.af.org.sa/node/10029
  • Imechapishwa: 14/02/2018