Takfiyr ya Raafidhwah kwa kila aliyezozana na ´Aliy (Radhiya Allaahu ´anh)


Wanawakufurisha wale waliopigana vita na ´Aliy (Radhiya Allaahu ´anh). Wakimkusudia ´Aaishah, Twalhah, az-Zubayr na wenzao na Mu´aawiyah na wenzao. Kumepokelewa mapokezi mengi kutoka kwake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) yanayofahamisha juu ya imani ya watu hawa na vile baadhi yao walivyobashiriwa Pepo. Kuwakufurisha ni kuyakadhibisha hayo. Wasipokuwa makafiri kwa ukadhibisha huu ni jambo lisilokuwa na shaka kwamba wanakuwa mafusaki. Hiyo inatosha kuwa ni khasara kwao katika biashara yao.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: ar-Radd ´alaa ar-Raafidhwah, uk. 73
  • Imechapishwa: 14/04/2017