Ahmad al-Ghumaariy amesema:

“Tambua kwamba Hadiyth zilizopokelewa juu ya watokaji ni zenye kufanana na Hadiyth za Khawaarij. Hata kama wote ni wenye kutoka katika dini (خوارج عن الدين) na wote ni mijibwa ya Motoni, kama alivosema Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), pamoja na hivo wamegawanyika mafungu mawili:

1 – Fungu la kwanza wanatambulika kwa jina hili. Wamesifiwa kuwa ni wenye kujikakama na kuchupa mpaka katika dini na kwamba mmoja wetu atazidharau swalah na swawm zake ukilinganisha na swalah na swawm zao.

2 – Fungu la pili ni wale wapotofu wa sasa (au wakanamungu wa zama hizi?!?!) (ملاحدة العصر). Wamesifiwa kuwa wapumbavu na vijana na kwamba alama zao ni kunyoa upara.

Pindi kulipozuka pembe ya shaytwaan huko Najd mwishoni mwa karne ya kumi na fitina yake ikaenea, basi wanachuoni wote walikuwa wakizitumia Hadiyth hizi juu yake na wafuasi wake, kwa sababu kulikuwa hakujazuka aina ya Khawaarij hawa hapo kabla.”[1]

Pili: Anamkusudia Shaykh Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab na katika kitabu hichohicho[2] amewaita watu wa Najd “wenye pembe” (القرنيون). Huu ni uongo na dhambi ya wazi kwa njia ya kwamba anawasifu kwa njia ambayo haiendani na wao bali inaendana na wengine. Allaah (Ta´ala) amesema:

وَالَّذِينَ يُؤْذُونَ الْمُؤْمِنِينَ وَالْمُؤْمِنَاتِ بِغَيْرِ مَا اكْتَسَبُوا فَقَدِ احْتَمَلُوا بُهْتَانًا وَإِثْمًا مُّبِينًا

“Na wale wanaowaudhi waumini wa kiume na waumini wa kike pasi na wao kufanya kosa lolote, basi kwa hakika wamejibebea uzushi mkuu wa dhuluma na dhambi ya wazi.”[3]

Abud-Dardaa´ ameeleza kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Yule mwenye kumtaja mtu kwa kitu asichokuwa nacho kwa lengo la kumuaibisha, basi atazuiwa Motoni mpaka pale atapotoa ushahidi wa yale aliyoyasema.”[4]

Ibn ´Umar ameeleza kuwa Mtume wa Allaah  (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Yule mwenye kusema juu ya muumini yale asiyokuwa nayo, basi Allaah atamnywesha usaha wa watu wa Motoni mpaka atoke nje ya yale aliyoyasema.”[5]

[1] Mutwaabaqat-ul-Ikhtara´aat al-´Asriyyah, uk. 76

[2] Ukurasa wa 50 hadi 127.

[3] 33:58

[4] at-Twabaraaniy katika ”al-Awsatw” (8/380). Nzuri kwa mujibu wa Ibn-ul-Mundhir.

[5] Ahmad, Abu Daawuud na at-Twabaraaniy ambaye ana nyongeza isemayo:

“… jambo ambalo hawezi kulifanya.”

  • Mhusika: ´Allaamah Hamuud bin ´Abdillaah at-Tuwayjiriy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Iydhwaah-ul-Mahajjah, uk. 138-139
  • Imechapishwa: 06/07/2020