Ibn-ul-Qayyim anasema kuwa hawa Jahmiyyah, Fir´awniyyah, Raafidhwah na wengine wameshuhudilia ukafiri kwa yule mwenye kuthibitisha kuonekana kwa Allaah Aakhirah na kusema ni katika watu wenye kumfananisha Allaah na viumbe Vyake [Mushabbihah] na wenye kumfanya Allaah kuwa na mwili [Mujassimah] kwa sababu wamemshabihisha Allaah na viumbe Vyake. Kwa sababu wanasema kuwa kinachoonekana ni kile kitu kilicho na mwili na kinakuwa na kikomo na kiwiliwili. Kuhusiana na Mola haonekani kwa sababu hana mwili na hana kikomo na hana sehemu ya kumfanya akawa na kikomo. Hivi ndivyo wanavosema. Wanasema kuwa yule mwenye kuthibitisha kwamba Allaah yuko juu na kwamba Allaah ana sehemu na akathibitisha kuwa ataonekana Aakhirah, huyo ni kafiri kwa kuwa ni Mushabbih na Mujassim. Kujengea juu ya hili Ahl-ul-Bid´ah wenye gonjwa hili wanawakufurisha Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Hidaayah ar-Rabbaaniyyah fiy Sharh al-´Aqiydah at-Twahaawiyyah (01/225-226)
  • Imechapishwa: 18/05/2020