Takfiyr kwa mtu wa kawaida


Swali: Je, inafaa kwa mtu wa kawaida kumkufurisha mwenye kufanya ukafiri?

Jibu: Kukithibiti kwake ukafiri anakufurisha. Kizuizi kiko wapi? Kukithibiti kwake yenye kuepelekea katika kufuru anamkufurisha. Kwa mfano tunamkufurisha Abu Jahl, Abu Twaalib, ´Utbah bin Rabiy´ah na Shu´bah bin Rabiy´ah. Dalili zimeonyesha kuwa wamekufa juu ya ukafiri hali ya kuwa ni makafiri na Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akawapiga vita siku ya Badr.

Swali: Wako ambao wanamkataza mtu wa kawaida kukufurisha. Ni ipi hukumu?

Jibu: Mtu wa kawaida asikufurishe isipokuwa kwa dalili. Mtu wa kawaida hana elimu ya kitu maalum. Akiwa na elimu ya kitu maalum kama mfano wa mwenye kupinga uharamu wa zinaa, mtu kama huyu anakufurishwa na mtu wa kawaida na ambaye ni msomi. Kwa sababu hakuna shubuha. Hakuhitajii dalili. Au kama akisema kwamba inafaa kwa watu kumwabudu asiyekuwa Allaah. Kuna yeyote anayetilia shaka jambo hili? Hakuhitajii dalili. Akisema kwamba inafaa kwa watu kuyaabudu masanamu, nyota au majini au akasema kwamba si lazima kuswali na kwamba mwenye kutaka, aswali, na asiyetaka, anaacha. Mwenye kusema mambo haya anakufuru. Mtu anatakiwa kunyamaza juu ya mambo yenye kutatiza ambayo yanaweza kufichikana kwa ambaye si msomi.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Kashf-ish-Shubuhaat, uk. 34
  • Imechapishwa: 11/06/2019