Takfiyr kwa Ashaa´irah?


Swali: Ikiwa Ashaa´irah wanasema kuwa Allaah (´Azza wa Jalla) Hazungumzi kwa sauti wala herufi, wanapinga Sifa za Allaah (´Azza wa Jalla), wanasema kuwa Allaah Yuko kila mahala na mengineyo katika ´Aqiydah zao mbovu. Je, wanakuwa ni makafiri kwa hayo?

Jibu: Wanafuata kichwa mchunga na wanaweka taawili. Hawapachikwi kufuru. Lakini wanapachikwa upotevu. Wanapachikwa ya kwamba ni wapotevu kwa kuwa wanaweza kuwa wanafuata kichwa mchunga au wajinga wanafuata yale waliyowakuta wengine.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Zaad-il-Ma´aad (62) http://www.alfawzan.af.org.sa/node/13740
  • Imechapishwa: 16/11/2014