Takfiyr kwa anayemtuhumu ´Aaishah (Radhiya Allaahu ´anha) uzinzi


Swali: Nikiashiria kwa mtu binafsi ambaye anamtukana mama ´Aaishah (Radhiya Allaahu ´anha) na kusema kwamba ni kafiri na ni mnafiki, je, kitendo hichi kinajuzu au ni katika kupetuka mipaka?

Jibu: Hii ndio hukumu yake. Lakini ikiwa katika kutangaza hilo kutapatikana madhara, basi usiseme hili wazi wazi kwa kuzuia fitina:

وَلَا تَسُبُّوا الَّذِينَ يَدْعُونَ مِن دُونِ اللَّـهِ فَيَسُبُّوا اللَّـهَ عَدْوًا بِغَيْرِ عِلْمٍ

“Na wala msiwatukane wale wanaowaomba asiyekuwa Allaah; wasije (nao) kumtukana Allaah kwa uadui bila ya kujua.” (06:108)

Isitoshe ikiwa katika kufanya hivi unaeneza uchafu huu, haijuzu kufanya hivi. Badala yake achana naye.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Zaad-il-Ma´aad (31) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/mo--1431-10-10.mp3
  • Imechapishwa: 15/11/2014