Takbiyr baada ya swalah


Swali: Wako watu ambao wanasema:

“Allaahu Akbar.”

baada tu ya kutoa Tasliym ya swalah kabla ya kuleta Istighfaar. Je, hili ni jambo limewekwa katika Shari´ah?

Jibu: Hapana. Haikuwekwa katika Shari´ah kuleta Takbiyr baada ya kutoa salamu ya swalah. Kilichowekwa katika Shari´ah ni kumdhukuru Allaah kwa kuleta “Tamhiyd, “Tahliyl” na “Tasbiyh”. Haya ndio yaliyopokelewa.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Ighaathat-il-Lahfaan (88) https://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/igahssat.mp3
  • Imechapishwa: 18/09/2018