Swali: Nikiingia msikitini na swalah ikakimiwa, inafaa kwangu kuswali Tahiyyat-ul-Masjid Rak´ah mbili za harakaharaka kisha ndio nijiunge na mkusanyiko?

Jibu: Hapana:

“Kunapokimiwa swalah basi hakuna swalah nyingine isipokuwa ile ya wajibu.”[1]

Hadiyth ni Swahiyh.

Haijuzu kwako kuswali swalah nyingine isipokuwa ile iliyokimiwa.

[1] Muslim (710).

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Ighaathat-il-Lahfaan (68) http://alfawzan.af.org.sa/node/16495
  • Imechapishwa: 23/07/2017