Tahiyyat-ul-Masjid kwa mtazamo wa wanachuoni


Swali: Kuna watu ambao hawaswali zile Rakaa´ mbili za Tahiyyat-ul-Masjid wakati wanapoingia msikitini. Ni ipi hukumu ya hilo?

Jibu: Dogo liwezalo kusemwa ni machukizo. Tahiyyat-ul-Masjid ni wajibu kwa maoni ya baadhi ya wanachuoni kama Dhwaahiriyyah. Wanachuoni wengi wanaonelea kuwa imependekezwa.

Kwa hivyo haitakikani kwa mtu anapoingia msikitini ilihali ana wudhuu´ akaketi chini. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema katika Hadiyth Swahiyh:

“Anapoingia mmoja wenu msikitini basi asiketi mpaka aswali Rakaa´ mbili.”

Lililo dhahiri ni uwajibu. Lakini akiwa hana wudhuu´ jambo lake ni pana.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (03) http://audio2.islamweb.net/lecturs/aalrrajhee/430/430.mp3
  • Imechapishwa: 08/04/2018