Swali: Vipi hali ya Swaalih bin ´Awwaab al-Mughaamisiy ambaye ni imamu wa msikiti wa Qubaa´ na ana darsa katika somo la tafsiri ya Qur-aan?

Jibu: Mtu huyu ni mjinga. Simshauri mtu kuchukua elimu kutoka kwake. Kwa sababu si mtu ametakhasusi katika elimu ya Shari´ah kutokana na khabari zilizonifikia. Hili ni mosi.

Pili ni mtu ambaye analingania katika madhehebu ya Suufiyyah[1]. Kitu kinachonifahamisha hilo ni kisa cha “al-Maqbuura”. Nimemraddi katika sahab.net kwa anwani “at-Taqriyraat al-Mastwuur”. Kisa hiki upande wa mlolongo wa wapokezi ni chenye kuanguka. Amekitoa kutoka kwa mwanachuoni moja wapo wa Taswawwuf ambaye amepindukia. Ni kisa kina mambo ya munkari mengi. Arejee huko yule anayetaka.

Nimefikiwa na khabari ya kwamba amesema kuwa inafaa kuacha baadhi ya mambo ya dini kwa ajili ya kutafuta umoja. Akimaanisha kwa mfano kuacha Tawhiyd au kukataza shirki kwa sababu ya kutafuta umoja. Hili al-Qaradhwaawiy alikuwa ameshamtangulia. al-Qaradhwaawiy ni kiongozi  aliyepindukia kabisa katika upotevu. Si kiongozi anayelingania katika uongofu. Ana mambo ya kufuru. Lau ningesema maneno haya aliyoyasema al-Qaradhwaawiy basi ningekufuru.

Kwa hivyo ni wajibu kwa watu kutahadhari na Swaalih bin ´Awwaab; ambaye ni imamu wa msikiti wa Qubaa´ kama ambavyo vilevile ni wajibu kutahadhari na al-Qaradhwaawiy na kutahadharisha wote wawili.

[1] Tazama https://firqatunnajia.com/taswawwuf-zote-ni-mbaya/

  • Mhusika: Shaykh ´Ubayd bin ´Abdillaah al-Jaabiriy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://www.youtube.com/watch?v=tH_ar2erh7E
  • Imechapishwa: 16/03/2018