Tahadhari na al-Jazeera!


Swali: Ni ipi hukumu ya chaneli ya al-Jaziyrah na inahalalisha Aliyoharamisha Allaah na kuharamisha Aliyohalalisha Allaah?

Jibu: Mi nimeshawaambieni tahadharisheni watu na chaneli hizi. Inahusiana na chaneli zote na sio al-Jaziyrah peke yake. Zimewasababishia Waislamu shari tupu. Watahadharisheni na chaneli zote. Mwenye kutaka barnamiji za kidini zinapatikana kwenye idhaa ya Qur-aan. Idhaa hii ina kheri nyingi, mawaidha, fataawa, taarifa ya khabari na mengine. Mwenye kutaka kheri inapatikana.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Aqiydat-is-Saffaariniyyah (13) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/sfranih_13.mp3
  • Imechapishwa: 20/06/2018