Swali: Mimi ni kijana ambaye nachelea fitina juu ya nafsi yangu ambaye natamani sana kuoa. Nina pato ambalo si baya. Baba yangu pia ni muweza. Nimezungumza na familia yangu mara nyingi lakini kuhusiana na jambo hili, lakini jibu lao siku zote ni kwamba ndoa ni jukumu na amana kubwa na kwamba yale yaliyonifanya nikasubiri muda wote huu mrefu yatanifanya kuweza kusubiri mpaka nitakapomaliza masomo yangu ya chuo kikuu na nikaajiriwa kazi. Naomba ushauri wako juu ya jambo langu, naomba umpe nasaha baba yangu na mimi pia pamoja na kuzingatia kwamba mimi ni muweza wa kuoa na naweza kujihudumia mimi mwenyewe na mke wangu na nyumba ni kubwa. Lakini hakuna kilichobaki isipokuwa tu kukubali kwa wazazi wangu.

Jibu: Nasema: mtegemee Allaah. Katika sehemu ya usiku mtafute mke. Usiwatii wazazi wako. Hapa kuna maamrisho mawili:

1- Amri ya baba yako kwamba usubiri.

2- Amri ya Mtume wako juu ya kutafuta mke. Ni amri ipi unayotakiwa kutanguliza? Ni amri ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliyesema:

“Enyi kongamano la vijana! Yule katika nyinyi atakayeweza kuoa basi aoe.”

Mtu huyu kwa mujibu wa swali lake ni mwenye uwezo; yuko na pesa, nyumba na kila kitu. Hivyo basi aoe. Akitosheka na mke mmoja ni sawa. Vinginevyo aongeze mke wa pili. Asipotosheka na wake wawili aongeze mke wa tatu. Asipotosheka na wake watatu aongeze mke wa nne. Asipotosheka na wake wanne, basi anunue kijakazi. Wajakazi achukue anaotaka.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa´ ash-Shahriy (65) http://binothaimeen.net/content/1466
  • Imechapishwa: 13/01/2020