Swali: Nikiwa na haja kubwa ya mbwa wa ulinzi na siwezi kumpata kwa njia nyingine isipokuwa kumnunua. Je, katika hali hii yule muuzaji ndiye anapata  dhambi?

Jibu: Hatufungui mlango huu. Kila mmoja atataka kuingia kupitia mlango huo. Haijuzu kumuuza mbwa. Mbwa anaweza kutumiwa pasi na kuuzwa. Mijibwa ni mingi. Tafuta mbwa kisha wewe mwenyewe mfunze.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (27)
  • Imechapishwa: 18/04/2021