Tafsiri ya al-Baraa´ kwa Ibaadhiyyah wanayowafanyia Maswahabah wakubwa kama ´Uthmaan (Radhiya Allaahu ´anh)

Kupitia vyanzo aminifu utapata kujua kuwa Ibaadhiyyah wanatangaza kwa wazi kabisa al-Baraa´ kwa kundi ambalo si dogo la Maswahabah wa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), kama itavyokuja upambanuzi wake huko mbele. Wanathibitisha hilo wale [wanachuoni wao] wa kale na wa sasa kwa kuwaiga wahenga wao Khawaarij. Wanahuisha fitina ambazo Allaah amewastarehesha waislamu kutokamana nazo. Wanayatambua hayo wale vichekechea vyao katika mitaala chini ya milango wanayoita “al-Walaa´ wal-Baraa´”, ambayo ni miongoni mwa misingi ya madhehebu ya Ibaadhiyyah. Hakuna anayewapinga juu ya hilo ingelikuwa ni kwa mujibu inavyojulikana katika Qur-aan katika kuwapenda waumini na kuwachukia makafiri. Huu ni msingi wa Uislamu uliyothibitishwa. Lakini wao wanaufanya msingi huu kuwa ni upenyezi wa kutangaza al-Baraa´ kwa Maswahabah na maimamu wakubwa wa Uislamu. Khaswa ukizingatia ya kwamba al-Baraa´ hii – kama inavyotambulika kwao na kutakuja upambanuzi wa hilo huko mbele – inamaanisha kuchukia kwa moyo, kulaani na kutukana kwa mdomo, kupambana kwa viungo vya mwili na kutekeleza kila aina ya uadui.

  • Mhusika: Abuu Swaalih Mustwafaa ash-Sharqaawiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Kuntu ibaadhwiyyaa yaa layta qawmiy ya´lamuun, uk. 4
  • Imechapishwa: 11/06/2017