Tabarruk kupitia mimbari ya Mtume

Swali: Ni ipi hukumu ya kubusu chumba cha kaburi la Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na kadhalika kufanya Tabarruk kwa kugusa mimbari yake?

Jibu: Mimbari imeumbwa na ni udongo. Kinachotakiwa kufanyiwa Tabarruk ni kile kilichogusana na mwili wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), kama mfano wa nywele na jasho. Haya ndio yanayofanyiwa Tabarruk. Kuhusu yale ambayo hayakugusana na mwili wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) hayafanyiwi Tabarruk.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Fath-il-Majiyd (87) https://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/fathoumaged05-03-1440h.mp3
  • Imechapishwa: 03/05/2019