Taarifu batili ya ni nani Swahabah


Swali: Siku hizi kumejitokeza mtu muovu anayewatukana Maswahabah na kusema kuwa Maswahabah ni wale waliosilimu kabla ya mji wa Makkah kutekwa. Kuhusiana na aliyesilimu baada ya Makkah kutekwa, huyo sio Swahabah. Je, maelezo yake ni sahihi?

Jibu: Haya ni maneno batili. Huyu ni muovu na ni Mulhid – na tunaomba kinga kwa Allaah. Anataka kubadilisha ´Aqiydah ya Waislamu. Watu hawa wameiponda ´Aqiydah, wamewasema vibaya maimamu na wamemtukana Imaam Ahmad na wengine. Si Maswahabah peke yake. Huyu ana chuki juu ya Uislamu wote. Anataka kuwatia mashaka Waislamu katika Dini yao na kueneza unafiki na ukafiri. Ni wajibu kutahadhari na mtu huyu na kujitenga naye mbali. Kuna kundi la wanachuoni limemraddi na himdi zote ni za Allaah. Wamebatilisha propaganda zake na kuvunja utata wake.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Aqiydat-is-Saffaariniyyah (12) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/sfranih_12.mp3
  • Imechapishwa: 23/06/2018