Swawm yako haikuwa sahihi


Swali: Miaka iliyopita niliacha kufunga masiku kadhaa ya Ramadhaan. Sijui ni masiku mangapi yaliyonipita. Ni kipi kinachonilazimu sasa pamoja na kuzingatia ya kwamba sikuwa mtu wa dini na nilikuwa naswali wakati fulani tu?

Jibu: Swawm yako si sahihi ikiwa ulikuwa mwenye kuacha swalah. Ni wajibu kwako kutubu kwa Allaah (´Azza wa Jall) na kuichunga dini yako katika mustakabali wa maisha yako.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Ighaathat-il-Lahfaan (85) http://alfawzan.af.org.sa/ar/node/17635
  • Imechapishwa: 29/06/2018