Swawm ya sunnah inafaa kwa mfungaji kufungua akitaka


Swali: Inajuzu katika funga ya sunnah mfungaji kula wakati anapotaka?

Jibu: Ndio, inafaa kwake kufanya hivo. Lakini bora ni yeye kukamilisha swawm yake. Isipokuwa kukiwa kuna haja ya kuikata kama vile kumkirimu mgeni, jua kali na mfano wa hayo. Kwa sababu imethibiti kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kupitia kwa ´Aaishah yanayofahamisha yale tuliyoyataja.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (15/420-421)
  • Imechapishwa: 09/06/2018