Swawm ya siku tatu kwa mwezi na alkhamisi na ijumaa tatu kuangukia siku ya shaka


Swali: Mwenye kufunga mwezi wa Sha´baan aunganishe na Ramadhaan au ni lazima atofautishe kati yake? Kwa mfano mtu ana mazowea ya kufunga siku tatu kila mwezi ambapo swawm yake ikachelewa na akawa amebaki na kesho na kesho yake. Je, anapata dhambi akifunga?

Jibu: Hapati dhambi akifunga. Hili linaingia katika maneno ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“… isipokuwa mtu ambaye alikuwa akifunga swawm. Basi aiendeleze.”

Kwa sababu Hadiyth isemayo:

“Asiitangulizie mtu Ramadhaan kwa kufunga siku moja au mbili isipokuwa mtu ambaye alikuwa akifunga swawm. Basi aiendeleze.”

Kwa mfano ikiwa mtu ana mazowea ya kufunga alkhamisi, katika mwaka huu huenda siku ya alkhamisi ikaaungukia siku ya mwisho ya Sha´baan, basi katika hali hiyo afunge ni sawa. Kadhalika yule ambaye haikumkuwia wepesi kufunga siku tatu kabla ya mwezi huu isipokuwa katika siku hizi, basi ni sawa akafunga. Kwa sababu yanaingia katika maneno yake:

“…isipokuwa mtu ambaye alikuwa akifunga swawm. Basi aiendeleze.”

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa´ ash-Shahriy (41) http://binothaimeen.net/content/1502
  • Imechapishwa: 14/05/2018