Swali: Ni ipi hukumu ya kufunga swawm za sunnah kama siku sita za Shawwaal, siku kumi za Dhul-Hijjah na siku ya ´Aashuuraa´ kwa yule ambaye anadaiwa baadhi ya masiku ya Ramadhaan na hajayalipa?

Jibu: Lililo la wajibu kwa yule ambaye anadaiwa masiku ya Ramadhaan aanze kuyalipa kwanza kabla ya kuingia kwenye swawm za sunnah. Kwa sababu swawm ya faradhi ina umuhimu zaidi kuliko swawm ya sunnah.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Tuhfat-ul-Ikhwaan, uk. 173
  • Imechapishwa: 02/06/2019