Swawm ya mzazi ambaye damu yake mchana imekatika na ikarudi usiku


Swali: Kuna mwanamke alizaa na damu yake ikakatika miezi mitatu baada ya kuzaa. Katikati ya usiku akajiwa na damu kidogo. Katikati ya mchana damu ikakatika na akafunga siku mbili. Damu ikarudi kwa mara nyingine na akaingia katika ada yake ya kila mwezi. Je, swawm ya siku zake mbili hizi ambayo alitokwa na damu katikati ya usiku inasihi?

Jibu: Ikiwa mambo ni kama ulivyotaja ya kwamba damu ilimtoka katikati ya usiku peke yake, basi funga ya siku zake mbili hizi ni sahihi. Kutokwa na kurudiliwa na damu katika nyusiku zote mbili hizi haiathiri.

  • Mhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa al-Lajnah ad-Daaimah (10/150)
  • Imechapishwa: 02/06/2017