Swawm ya mjamzito anayetokwa na majimaji

Swali: Kuna mwanamke Ramadhaan ilimfikia akiwa mjamzito katika mwezi wa tisa. Mwanzoni mwa mwezi alikuwa akitokwa na maji na sio damu. Alikuwa akifunga wakati maji hayo yanamtoka. Haya yalitokea miaka kumi iliyopita. Je, ni wajibu kwa mwanamke huyu kulipa siku hizi pamoja na kujua ya kwamba alifunga masiku haya na maji yakimtoka?

Jibu: Mambo yakiwa kama yalivyotajwa swawm yake ni sahihi na wala hana juu yake kulipa.

  • Mhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa al-Lajnah ad-Daaimah (10/221)
  • Imechapishwa: 10/06/2017